Revelation of John 13

1Kisha nikaona mnyama akitoka kwenye bahari. Alikuwa na pembe kumi na vichwa saba. Katika pembe zake kulikuwa na taji kumi, na katika kichwa chake kulikuwa na maneno ya kufuru kwa Mungu. 2Huyu mnyama niliyemuona ni kama chui. Miguu yake ilikuwa kama ya dubu, na mdomo wake ulikuwa kama wa simba. Yule joka akampa nguvu, na katika kiti chake cha enzi, na mamlaka yenye nguvu sana ya kutawala.

3Kichwa cha mnyama mmojawapo kilionekana kuwa na jeraha kubwa ambalo lingesababisha mauti yake. Lakini jeraha lake likapona, na dunia yote ikashangazwa na ikamfuata mnyama. 4Pia wakamwabudu joka, maana alimpa mamlaka yule mnyama. Wakamwabudu mnyama pia, na wakaendelea kusema, “Nani kama mnyama? na “Nani atapigana naye?”

5Mnyama akapewa mdomo ili azungumze maneno ya kujisifu na matusi. Aliruhusiwa kuwa na mamlaka kwa miezi arobaini na miwili. 6Hivyo mnyama alifungua mdomo wake kuongea matusi dhidi ya Mungu, akalitukana jina lake, eneo alililokuwa akiishi na wale wanaoishi mbinguni.

7Mnyama aliruhusiwa kufanya vita na waamini na kuwashinda. Pia, alipewa mamlaka juu ya kila kabila, watu, lugha na taifa. 8Wote walioishi duniani watamwabudu yeye, kila mmoja ambaye jina lake halijaandikwa, toka uumbaji wa dunia, katika kitabu cha uzima, ambacho ni cha Mwana Kondoo, ambaye alichinjwa.

9Ikiwa yeyote ana sikio, na asikilize. 10Ikiwa mmojawapo amechukuliwa mateka, na kwenye mateka ataenda. Ikiwa mmojawapo ataua kwa upanga, kwa upanga atauawa. Huu ni mwito wa utulivu na uvumilivu na imani kwa hao walio watakatifu.

11Tena nikaona mnyama mwingine anakuja kutoka katika nchi. Alikuwa mwenye pembe mbili kama kondoo na akazungumza kama joka. 12Alionyesha mamlaka yote katika mnyama yule wa kwanza katika uwepo wake, na kufanya katika dunia na wale walioishi wakimuabudu yule mnyama wa kwanza, yule ambaye jeraha lake limepona.

13Akafanya miujiza yenye nguvu, hata akafanya moto ushuke katika dunia kutoka mbinguni mbele ya watu, 14na kwa ishara aliruhusiwa kufanya, akawadanganya hao wakaao katika dunia, akiwaambia kutengeneza sanamu kwa heshima ya mnyama ambaye alikuwa amejeruhiwa kwa upanga, lakini bado aliishi.

15Aliruhusiwa kutoa pumzi katika ile sanamu ya mnyama ili sanamu iweze kusema na kusababisha wale wote waliokataa kumwabudu mnyama wauawe. 16Pia akalazimisha kila mmoja, asiye na thamani na mwenye nguvu, tajiri na maskini, huru na mtumwa, kupokea alama katika mkono wa kuume au katika paji la uso. 17Ilikuwa haiwezekani kwa kila mtu kuuza au kununua isipokuwa mwenye alama ya mnyama, na hii ni namba yenye kuwakilisha jina lake.

Hii inahitaji busara. Ikiwa yeyote ana ufahamu, mwache aweze kufanya hesabu ya namba ya mnyama. Maana ni namba ya kibinadamu. Namba yake ni 666.

18

Copyright information for SwaULB